MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
amefunguka kuwa watu wanaomsema vibaya
kuhusu yeye kupewa kichapo na mpenzi wake,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wanakosea kwani
anaamini kufanywa hivyo ni mahaba.
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda
akiwa na mpenzi wake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii hivi
karibuni, Mziwanda alisema kuna taarifa zimeenea
kuwa huwa anapigwa na Shilole pindi anapokosea
lakini ukweli si kupigwa ‘live’ bali ni kupigwa
kimahaba.
“Jamani kupigwa wanakozungumzia watu sielewi
lakini mimi ananipiga kimahaba, wanaosema kuwa
mpenzi wangu ananipiga washindwe, watuache kwa
raha zetu,” alisema Shilole.
Post a Comment