Featured

    Featured Posts

Walimu Wawili Wakamatwa Wakituhumiwa KUVUJISHA Mtihani wa kidato cha nne

Walimu wawili wa Shule ya Sekondari ya
Embarway wanashikiliwa na polisi wilayani
Ngorongoro wakituhumiwa kufanya mtihani wa
kidato cha nne ofisini.
Licha ya walimu hao kukamatwa pia waliokuwa
wasimamizi  wa ndani wa mitihani kwenye shule
hiyo, wameondolewa kutokana na uzembe.
Kaimu ofisa elimu wa Wilaya ya Ngorongoro,
Chacha Megewa alidai walimu hao, Jakob Jadie
na Reginald Boniface, walikamatwa wakati
wakifanya mtihani wa historia.
Alisema walikamatwa Novemba 5 walikamatwa na
msimamizi mkuu wa mitihani, Faustine Bura baada
ya kuingia ghafla katika ofisi ya mwalimu mkuu.
“Msimamizi alikuwa anafuata moja ya fomu ofisi ya
mkuu wa shule, baadaye aliita polisi na
kuwakamata,” alisema.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas jana hakupatikana kuelezea tukio hili, lakini
polisi Kituo kidogo cha Ngorongoro ilithibitisha
kukamatwa kwa walimu hao.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Featured Posts

Recent Posts

About us

Popular Posts

Translate

Total Pageviews

Copyright © jaka classic | Designed By Code Nirvana