ulimwengu
zinaendelea kukaa kwenye headlines kila
siku, na inaponifikia cha kwanza
ninachokifanya ni kukufikishia mapema
iwezekanavyo ili na wewe usipitwe.
Ya leo inaweza kuwa moja kati ya
zilizowahi kukushangaza zaidi, inahusu
mwanamke Janina Kolkiewicz raia wa
Poland, mwenye umri wa miaka 91
ambaye amekaa kwa muda saa 11
katika chumba cha kuhifadhia maiti huku
mwili wake ukiwa ndani ya jokofu baada
ya kuthibitishwa na daktari wa familia
yake kwamba amefariki, muda mfupi
baadaye wahudumu wa mochwari
waligundua kwamba ni mzima baada ya
kuhisi anatikisika ndani ya mfuko
alimowekwa.
Baada ya kurudi nyumbani kwake
akitokea mochwari, alilalamika kuhisi
baridi kali na kupatiwa bakuli la supu ya
moto na mkate.
Daktari aliyethibitisha mauti ya mtu huyo
anasema hata yeye anashangazwa na
tukio hilo kwani vipimo vyote vilionyesha
kuwa mapigo ya moyo yalisimama na
hakuwa hai.
Taarifa za kuwa hai mwanamke huyo
zilimshtua kila mtu kwenye familia yake
na kujikuta ikibatilisha hati ya kifo
iliyotolewa kwa ajili ya mazishi yake
ambayo yalipangwa kufanyika siku mbili
Post a Comment