LEO hii kwenye Live Chumba cha Habari ya
Global Publishers tunaye mwanamuziki Elly
Michael Kilema ‘Y Tony ’ kijana anayekuja kwa
kasi na wimbo wake unaofahamika kama
‘masebene’ anafanya vema sana kupitia staili
ya uimbaji wake .
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo Y -
Tony akiwa katika pozi ndani ya studio za
Global TV Online mara baada ya kuwasili kwa
ajili ya kufanyiwa mahojiano leo.
Katika mahojiano na safu hii huku akirekodiwa
na timu nzima ya Global Tv Online , Y - Tony
alisema staili yake ya uimbaji wa kulalamika
inatokana na watu wengi kuumizwa kwenye
mapenzi.Ifuatayo ni sehemu ya mahojiano
ambayo pia yanapatikana kupitia tovuti ya
www. globaltvtz.com
Mwandishi: Umekuwa ukipanda jukwaani na
jeneza. Je, wewe ni Freemason ?
Y Tony: Msanii anatakiwa awe mbunifu, hiyo ni
staili moja ya peke yangu inayonitambulisha
sehemu mbalimbali na msanii ili awe mzuri si
kwenye uimbaji tu hata kwenye kupafomu pia
kunawapa nguvu mashabiki ndiyo maana
nimeamua kuchagua staili ile.
Mwandishi: Wewe ni msanii mkubwa sana kwa
nini huwa hupati shoo kubwa unahisi tatizo ni
nini?
Y Tony: Watu walikuwa hawanijui hapo nyuma
lakini sasa hivi napata shoo kubwa kama
Fiesta na shoo za mamisi Morogoro na
nyingine nyingi kubwa.
Y- Tony wakati akifanyiwa mahojiano na
presenta wa Global TV Online , Pam Daffa
( kushoto).
Mwandishi: Mwaka jana ulichaguliwa kwenye
kategori ya msanii chipukizi ukiwa pamoja na
ukiwa pamoja na msanii Young Killer kuwania
tuzo za muziki za Kilimanjaro , ulijisikiaje ile
tuzo alivyoipokea Young Killer?
Y Tony: Unajua kila kitu kinapangwa ,
naamini nilikuwa naweza kuchukua mimi lakini
alivyochukua Young Killer nimeridhika pia yeye
alikuwa anasikika sana kwa sababu mimi watu
wengi wanaujua wimbo wangu na nina
mashabiki hadi watu wazima ambao siyo umri
wetu na ninapotunga wimbo sijiimbii mimi wala
mwanamke wangu naimba kwa jamii nzima
yaani mwanume inamhusu na mwanamke
inamhusu na yeyote atakayemfanyia ubaya
mwenzie nyimbo yangu inamhusu.
Mwandishi: Kuna picha ilikuwa kwenye
mitandao upo na msichana, ni mpenzi wako ?
Y Tony: Zile picha zilikuwa ni za kava kwa ajili
ya Cd ya wimbo mpya wa ‘ My Shitobe ’ vitu
vingine ni mapema mno kuvifahamu na siyo
vya kuweka hadharani na mimi ni mtu mzima
lazima niwe na mpenzi siku ikifika watu
watamfahamu.
Mwandishi wa Global Publishers Ltd , Musa
Mateja ( kushoto) akizungumza jambo na Y -
Tony muda mfupi baada ya kukamilisha
mahojiano hayo .
Mwandishi:
Unazungumziaje suala la vijana wadogo kuwa
na uhusiano wa kimapenzi na wanawake
wenye umri mkubwa ‘sugar mamy ’?’
Y Tony: Hilo halipo kwa vijana wadogo tu hata
watu wazima , mwanaume huwezi kulelewa na
mwanamke japokuwa siku hizi nao wanakuja
kwa kasi katika hilo .
Mwandishi: Ni usumbufu gani unaoupata kutoka
kwa wasichana ?
Y Tony: . Usumbufu upo lakini huwezi kusema
eti binadamu mwenzio anakusumbua.
Post a Comment