Msanii wa muziki Shetta amesema hana tatizo
lolote na Hemedy PHD, huku akidai kuwa huenda
kauli yake aliyosema kwa sasa hatafanya collabo
na wasanii wa ndani tena ilinukuliwa vibaya na
huenda ndo imemsababishia matatizo hayo.
Hemedy PHD hivi karibuni baada ya kusikia kauli ya
msanii huyo alitweet kuonyesha hakupendezwa na
kauli hiyo.
Akizungumza na bongo5 leo, Shetta amesema kuwa
kauli hiyo iliwakilishwa vibaya na vyombo vya
habari.
“Nilichokisema katika project yangu mpya itakayo
sitafanya collabo tena na msanii yoyote wa ndani
kwa upande wangu ila kama kuna mtu anataka
kufanya collabo na mimi milango ipo wazi, napenda
kuweka wazi hili,nimeshafanya nyimbo sita nikiwa
nimewashirikisha wasanii wa ndani, sasa huu ni
wakati wa kutanua wigo kwa upande wangu, mimi
binafsi sina tatizo na Hemedy, mimi nafikiri
alinielewa vibaya tu, uwakilishaji wa habari katika
vyombo vya habari waliwakilisha vibaya. Nitafanya
collabo na mtu yeyote atakayehitaji kufanya na mimi
kwenye project yake, lakini kwa wimbo nitakaotoa
mimi either nifanye mwenyewe au nifanye collabo
na msanii wa nje,” alisema Shetta.
Post a Comment