Featured

    Featured Posts

HII NDIO SIRI YA MMILIKI WA FACEBOOK KUVAA T.SHIRT YA AINA MOJA KILA SIKU

Hapa nyumbani Tanzania nimeshawahi
kusikia kuhusu matajiri wachache
wanaofanya biashara ambao huwa
hawabadili nguo zao au huwa kuna
vitu wanafanya vinavyopelekea hisia
za watu kuamini kwamba utajiri wao
ni wa uchawi.
Mfano kuvaa nguo ya aina moja
hiyohiyo kila wakati, wengine huwa
wanatembelea magari mabovu kabisa
lakini watoto wao na wake zao
wanatembelea magari makali na
wanabadilisha kila wakati, wengine
tunaambiwa wanalala barazani.
Sasa hii ya tajiri wa mtandao wa
kijamii wa Facebook wenye watumiaji
zaidi ya bilioni moja kote duniani
Mark Zuckerbeg sijui watu wataiweka
kwenye kipande gani manake
ameonekana mara nyingi sehemu na
nyakati tofauti akiwa amevaa Tshirt
moja tu ya kijivu.
Ni swali ambalo Waandishi wengi
waliwahi kutamani kupata time ya
kumuuliza ambapo kwa bahati nzuri
kaulizwa kwenye kipindi cha maswali
na majibu na akatoa jibu akiwa na
tabasamu zito kabisa.
‘Nimepata hii bahati ya kipekee kuwa
kwenye nafasi niliyonayo, ninaamka
kila siku na kuwahudumia zaidi ya
watu bilioni moja duniani… naona
sitofanya kazi yangu vizuri kama
nitatumia muda wangu kwenda
kutafuta/kuchagua nguo nzuri, tshirt
mnayoniona nayo ni ya rangi moja
lakini nilizinunua nyingi za namna
hii’
‘Ni Tshirt ambayo sio moja… ninazo
nyingi ila zinafanana, muda wangu
mwingi nimeutenga kwa ajili ya
kuhudumia watu na sio kujihudumia
mimi kwenye kuchagua nguo nzuri,
mavazi ni kitu kidogo sana kwangu’

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Featured Posts

Recent Posts

About us

Popular Posts

Translate

Total Pageviews

Copyright © jaka classic | Designed By Code Nirvana