Zikiwa ni takribani wiki tatu tangu tasnia
ya muziki wa injili nchini kumpoteza
mmoja wa waimbaji wake marehemu
mchungaji Debora Saidi, taarifa ambazo GK
imezipata ni kwamba mwimbaji mwingine
wa muziki wa injili Orida Njole amefariki
dunia mchana wa leo katika hospitali ya
Temeke jijini Dar es salaam alikokuwa
akipatiwa matibabu.
Orida ambaye mpaka umauti unamfika
mchana wa leo ilikuwa bado haijajulikana
nini hasa kinamsumbua lakini alikuwa
ameishiwa damu sana, mpaka umauti
unamkuta alikuwa anatamba na album
yake iitwayo 'Duniani tu wapitaji' huku kwa
mujibu wa watu waliomfahamu marehemu
wameeleza kwamba alikuwa mtu
mchangamfu wakati wote wakati wa uhai
wake na kwamba wamepokea kwa
masikitiko makubwa taarifa za kifo chake.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la
Bwana libarikiwe!
Picha ya mbele ya álbum ya marehemu
Orida Njole.
Marehemu Orida akiwa na mtoto yatima
katika kituo cha Tosamaganga Iringa
alipotembelea kituoni hapo
CHANZO:MATUKIO NA VIJANA
Post a Comment