Na Musa Mateja
MISS
Tanzania 2006/07 ambaye ni staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu
‘Gorgeous Onyinye’, amevunja ukimya kwa kuamua kuanika kisa cha yeye
kummwaga aliyekuwa mwandani wake, nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul
‘Shape Platnumz’.
Akizungumza
na Amani katika mahojiano maalum jijini Dar, juzikati, Wema alianza kwa
kufunguka kwamba, kuna watu wamekuwa wakizungumzia ishu ya yeye kumtema
Shape huku kisa wakiwa hawakijui na wengine wamehamishia sababu kwa
nyota wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’, jambo ambalo si kweli.
Wema
alimwaga ‘ubuyu’ kwamba, yeye ameamua kumpa likizo ndefu Shape ili kila
mmoja aweze kufanya mambo yake ya maana kwa uhuru mkubwa hasa baada ya
jamaa huyo kunukuliwa na magazeti pendwa akisema hana mpango wa kuoa
jambo ambalo lilimkatisha tamaa na kumwacha njia panda.
SAFARI YAKE CHINA NAYO TATIZO
Kuhusu suala la kusema amempa likizo ndefu ili kila mtu afanye mambo yake,
Wema
alirejea safari yake ya China hivi karibuni ambapo Shape hakutaka
asafiri ila akalazimisha. Hapo aliona anatakiwa kuwa huru zaidi.
MWISHO WA LIKIZO
Wema alipotakiwa kutaja mwisho wa likizo hiyo endapo ni ya siku 28 kama ilivyo
kwa sheria ya kazi ya Tanzania, aligoma kusema chochote huku akisisitiza amempa likizo Shape.
AMZUNGUMZIA ZARI
Staa
huyo asiyekaukiwa na matukio, alikwenda mbele zaidi kwa kumzungumzia
Zari ambapo alisema kuna wanaodai mwanamuziki huyo tajiri yuko kimapenzi
na Shape, lakini yeye haoni ukweli wowote kwani anajua wawili hao wana
‘projekti’ ambayo ni mawazo ya muda mrefu.
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
“Kwanza
naomba watu wajue kuwa, projekti ya Shape na Zari ninaijua na bahati
nzuri Zari ni shoga‘ngu tangu kitambo hivyo yote yanayofanyika mimi
nayatambua hatua kwa hatua pamoja na kwamba sijaongea na Shape siku
nyingi,” alisema Wema.
DIAMOND AULIZWA KAMA ANAITAMBUA LIKIZO NDEFU
Baada
ya mazungumzo na Wema, mwanahabari wetu alimtafuta Shape kwa lengo la
kutaka kumfahamisha kama anafahamu kwamba amepewa likizo ndefu.
“Dah!
Nashindwa niseme nini hapo! Lakini ujue maisha kila mfa maji siku zote
haishi kutapatapa, kiukweli mimi hapo naona Wema anatoa majibu ya
kisiasa tu.
“Nashindwa
kujibu kila linalosemwa na watu ila kuna kipindi mtu hutakiwi kujibu
kila kitu. Kuna mambo mengine yanatakiwa uyaache yapite tu.
“Mimi
nimeachwa na Wema, Zari ni rafiki yangu tu, acheni projekti iendelee,”
alisema Shape huku akichekacheka kwa ishara ya furaha akijiandaa kuachia
ngoma kali mpya iitwayo ‘Nitampata Wapi’ leo.
KWENYE WHATSAPP
Wakati
Shape akisema hayo, baadaye kwenye maelezo yake mafupi (profile) ya
WhatsApp aliweka picha ya Zari huku akiambatanisha na maneno
yaliyosomeka:
“Unapokosa usisikitike, Mwenyezi Mungu kakuandalia kizuri zaidi.”
Wema na Shape wamekuwa na kasumba ya kuachana na kurudiana hivyo kuna kila dalili wawili hao wakarudiana tena.

Post a Comment