MATOKEO YA HESABU YA LULU>>>AJBU CHEKA UVIMBE KWEL UZUR SIO AKILI TAZAMA TUUU NAWE UJIULIZE LULU HUYOO
Nilipokuwa shule ya msingi, kuanzia darasa la 4 hadi la 7 maksi zangu
za hesabu kwenye mitihani zilikuwa zinacheza kwenye 03%- 08%. Matokeo
yalikuwa yanatangazwa mbele ya darasa! Yanapotangazwa mwalimu anaanza
kuwaita wanafunzi kwa kuanzia maksi za chini kwenda juu (0-100), kwahiyo
darasa lote linajua makaratasi yakiletwa lazima niitwe kama si wa
kwanza basi wa pili toka chini. Siku moja mwalimu akaanza kuita majina,
mpaka akafikia kwenye maksi 30%,40%,50%,60%,70% bado tu mi hajaniita.
Watu wakaanza kuniangalia waliokuwa karibu wakaanza kuniuliza..."" Eeeh
umepasua hujaitwa, ilikuwaje?? Nlianza kuvimba kichwa, huku mwalimu
anaendelea kugawa tu makaratasi. Yakabaki makaratasi ya watu wawili tu
waliopata 80%-90% bado mi sijaitwa ... Mara akabaki na karatasi moja
mkononi...!!!! Darasa lote macho kwangu hawaamini kinachotokea maana
bado sijapata karatasi.. Mwishoni mwalimu akaangalia juu akashusha
pumzi, kisha akasema... "KUNA NG'OMBE hajaandika jina kapata 0% aje
kuchukua karatasi lake!!. Hahaaaaa ni shiderrrrrr
Post a Comment