Utafiti
uliofanywa na wanasayansi wa masuala ya afya na lishe nchini Marekani
umebaini kuwa “kifungua kinywa huupa moyo afya na kuuepusha na magonjwa
ya mshtuko wa moyo.”
Utafiti
wao uliowahusisha wanaume 27,000 wenye umri kati ya miaka 45-82
ulionyesha kuwa wale wasiokula kiamsha kinywa wako katika hatari ya
matatizo ya moyo. Wakati wa utafiti huo, zaidi ya watu 1,500
waliathirika kutokana na mshtuko wa moyo. Utafiti
huo ulithibitisha kuwa watu waliokosa kifungua kinywa wako katika
hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo kwa asilimia 27 kuliko wale
wanaokula asubuhi.
Ukizingatia utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Harvad kitivo cha afya ya jamii kilisema kuwa: “kukosa kiamsha kinywa kunasababisha mwili kutumia nguvu nyingi zaidi kuliko kawaida.” Sambamba na utafiti huo, taasisi ya matibabu ya moyo nchini Uingereza imebaini kuwa “kiamsha kinywa huwazuia watu kula vitu vyenye sukari kabla ya chakula cha mchana.”(

Post a Comment