Claudio Romani sasa amekuwa refa ambaye
amefuzu kuchezesha za Ligi Kuu na Daraja la
Kwanza Italia
MWANAMITINDO wa Italia, Claudia Romani
ameingia kwenye rani mpya katika ulimwengu
wa soka- baada ya kufaulu mtihani wa kuwa
refa wa kulipwa.
Kimwana huyo mwenye umri wa miaka 32
amevua viatu vyake vya mchuchumio ili awe
refa, kitu ambacho imekuwa agenda yake kwa
miezi kadhaa.
Romani sasa amefuzu kuwa refa wa mechi za
Ligi Kuu ya Italia maarufu kama Serie A na
Daraja la kwanza, maarufu kama Serie B - kitu
ambacho anaelewa vizuri.
Amesema: "Kukimbia uwanjani na wachezaji
wote hao na kuchezesha mechi ni nafasi
adimu,".
Hakuna mwanamke amewahi kuchezesha
mechi ya Serie A hadi sasa kutokana na
uzoefu, jambo ambalo linatarajiwa kubadilika
karibuni kwa Romani kutazamiwa kuwasha
moto katika ligi ya Italia
Post a Comment