
Akizungumzia jinsi alivyopokea taarifa za matokeo yake, Rachel alisema ni kwa furaha na alikuwa akitengemea kufaulu, lakini siyo kwa mafanikio kama hayo aliyoyapata.
“Nanamshukuru sana Mungu kwani nilikuwa namwomba atende maajabu katika matokeo yangu... nilikuwa nasali kila nikifanya mtihani na kumaliza,” alisema Rachel, ambaye alikuwa akiishi na bibi yake Kimara.
Aliwashukuru walimu wake wa masomo yote kwa juhudi za kuwafundisha vizuri wanafunzi wote katika shule hiyo kwani walikuwa wakiingia darasani kwa muda wa ziada na kutoka saa 11 jioni.
“Mimi nawashauri wanafunzi wenzangu tuliomaliza wote na kufaulu kuwa tuongeze bidii katika masomo yetu ya Sekondari kwani bila juhudi hatutaweza
Post a Comment