Featured

    Featured Posts

download nyimbo mpya ya jux

Shilole: Watoto Wangu Ndio Wananifanya Niende “Resi”

Mwigizaji na mwanamkizi, Zuena Mohammed
'Shilole' ambae ni mama wa watoto wawili,kama
mzazi leo hii amewandikia ujumbe mzito watoto
wake mara baada ya kubamdika picha yao hiyo
hapo juu.
“Hawa ndo wananifanya mm naenda resi kila siku!
Nawapenda sana watoto wangu! Rahma na joyce!
Shule ndo zishafunguliwa mkasome! Mtimize zile
ahad zenu! Hahahahaah Rahma kaniahid eti
ataninulia private jet! Wakati Joyce kaniahid
kunijengea nyumba yenye kila kitu ndani!
Hahhahahhh wanangu wanipa raha sana!...

Samaki huyu kafanyiwa upasuaji, gharama za upasuaji huo ni zaidi ya dola 400

RTXL007-950x646
Hizi ni moja ya story ambazo hatujazoea kuzisikia kwa watu kama wa Bongo, eti kutoa dola 400 kumtibia mnyama, tena samaki?
Kutoka Norfolk Uingereza, jamaa mmoja ametumia dola 465 kumtibu samaki wake aina ya Goldfish aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la tumbo ambapo alikuwa na tatizo katika mfumo wa kuyeyusha chakula.
Aligundua kwamba hali ya samaki wake sio nzuri, hakujua ukubwa wa tatizo, ila alipofika kwa mtaalamu wa masuala ya wanyama aliambiwa kinachotakiwa kufanyika, operation yote ikachukua kama dakika hamsini hivi.
245B4B7E00000578-2893453-image-a-32_1420116147984Daktari Faye Bethell ndiye aliyesimamia zoezi hilo la upasuaji na baadaye samaki huyo akashonwa nyuzi tatu.
245C342100000578-2893453-image-a-60_1420121047263
245B4B9000000578-2893453-image-m-38_1420116184149
245B4B3700000578-2893453-image-m-27_1420116115061
245B3D8300000578-2893453-image-a-17_1420116027634nmkhuj
245B3D8800000578-2893453-image-a-18_1420116037369jkmlo;
245B4B8B00000578-2893453-image-a-28_1420116118920llkk

Picha7 alivyofunika msanii Diamond nchini Rwanda siku ya mwaka mpya


 
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa amebebwa na wacheza shoo wake siku ya mwaka mpya Kigali, Rwanda.
 
Diamond Platnumz akifanya yake.
 
Nyomi ya kufa mtu waliofika siku ya shoo hiyo.
 
Akifanya yake na wacheza shoo wake.
 
Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari'  au 'The Boss Lady' mpenzi mpya wa Diamond Platnumz akiwa katika pozi.
 
Muonekano wa siku ya shoo hiyo.
 
Diamond Platnumz (katikati) akifanya yake akiwa na Yamoto Bendi.

Huyu ndie mwanafunzi aliehukumiwa kwenda jela kwa kosa la kumtukana Rais Kenyatta kwenye mtandao wa kijamii

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.
Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo chengine cha mwaka mmoja.
Alikuwa ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.
Mwanablogu mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.
Kenya ina mitandao mahiri na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema kuwa kesi hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu kile kilichosahihi katika mitandao.

ATANGAZA KUUZA FIGO KWA SHILINGI MILIONI 90!!!



Mkazi wa Morogoro, Andrew Germanis Chimulimuli ametangaza kuingiza sokoni figo yake ambayo amesema anaiuza Sh90 milioni ili kukabiliana na ugumu wa maisha.Chimulimuli aliyefunga safari kutoka Ifakara, Morogoro hadi jijini Dar es Salaam ili kufanya biashara hiyo alisema ameamua kutoa kiungo chake hicho muhimu kutokana na ugumu wa maisha unaomkabili.“Nimeamua kujitolea nafsi yangu ili niisaidie familia yangu, kwa sababu mimi si kitu kama sina fedha, ndiyo maana nimejitolea kutoa figo yangu nipate fedha,” alisema Chimulimuli.

Chimulimuli alisema anataka kuiuza figo hiyo kwa gharama ya Sh90 milioni ingawa alikubali kufanya mazungumzo ya kupunguza bei pindi atakapopatikana mteja.

Takwimu za Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii zinaeleza kuwa kuna wagonjwa 470,000 nchini ambao figo zao zimeshindwa kufanya kazi kabisa na wanahitaji upandikizaji.

Ingawa uamuzi wa Chimulimuli unaweza kuwa msaada kwa Watanzania wenye mahitaji, lakini kimaadili ya afya na kisheria, jambo hilo linakatazwa kufanywa kiholela hadi pale linapofuata taratibu.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Figo Tanzania, Jaji Frederick Werema aliwahi kuliambia gazeti hili kwamba anashangazwa na hatua za baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kuuza figo kwa ajili ya kujipatia fedha.

“Kutoa figo ni kosa la jinai, lakini siyo hivyo tu, kutoa figo ni lazima ufuate taratibu za kisheria na za kitabibu,” alisema Jaji Werema miezi kadhaa iliyopita.

Biashara ya figo

Aprili mwaka jana, gazeti hili lilifanya uchunguzi na kubaini kuwa wapo Watanzania wanaouza figo zao kiholela kwa ajili ya kujipatia fedha.

Gazeti hili liliwasiliana na vijana kadhaa ambao kwa nyakati tofauti walikubali kuwa wanauza figo zao na baadhi wakieleza kuwa tayari walishauza kwa gharama za kati ya Sh50 milioni hadi Sh80 milioni.

Chimulimuli alisema kutokana na ugumu wa maisha, kipato chake kimekuwa kigumu sana na hakiwezi kukidhi mahitaji ya familia.

“Mtu akikuona kwa nje anaweza kukuona kama upo sawa na una maisha mazuri lakini ukweli ni kuwa nina maisha magumu sana,” alisema. Kuhusu hatima yake kiafya, alisema yeye ni msafiri na hawezi kuishi milele na hivyo bora auze figo yake iwe msaada kwa wengine wenye mahitaji.

“Ni bora nifanye kitu cha halali kinachoigharimu afya yangu mwenyewe badala ya kuiba au kufanya uhalifu mwingine,” alisema Chimulimuli.

Uchangiaji wa figo

Daktari bingwa wa figo katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Linda Ezekiel alisema uchangiaji wa figo ni mchakato mrefu na si suala la fedha tu.

Dk Ezekiel alisema mchakato wa kuchangia figo ni mrefu kwani mchangiaji hutakiwa kuwa na kundi la damu linalofanana na mgonjwa.

Alisema vipimo vya afya hufanyika ambapo maradhi yanayoweza kuambukiza kama homa ya ini, magonjwa ya zinaa na Virusi vya Ukimwi, navyo huangaliwa kwa umakini mkubwa.

“Ni lazima tuhakikishe mtu ameridhia kabisa kufanya hivyo na katika hali hiyo ni lazima tumfanyie mtu ushauri wa kisaikolojia na afahamu hatua za utoaji huo sambamba na madhara anayoweza kuyapata,” alisema.

Kuhusu changamoto ya maradhi hayo Dk Ezekiel alisema kusafisha figo ‘dialysis’ ni gharama kubwa ambapo kwa tiba moja mgonjwa hutakiwa kulipa Sh300,000 na tiba hiyo hufanywa angalau mara tatu kwa wiki.

Hata hivyo Dk Ezekiel alisema kwa anayechangia figo na kubaki na moja hawezi kupata madhara kiafya kwani figo moja ina uwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.

www.CodeNirvana.in

Featured Posts

Recent Posts

About us

Popular Posts

Translate

Total Pageviews

Copyright © jaka classic | Designed By Code Nirvana